Badilisha Mafuta ya Injini
Tazama Kielelezo: 15, 16, 17, 18
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa
moto zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
• Unapomwaga mafuta kutoka kwenye bomba la juu la kuweka mafuta, tangi ya
mafuta lazima iwe tupu au mafuta yanaweza kumwagika nje na kusababisha moto
au mlipuko.
• Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
Kagua na uongeze mafuta kama inavyotakikana. Tazama sehemu Kuangalia
Kiwango cha Mafuta. Hauhitaji kubadilisha mafuta lakini ukitaka kubadilisha mafuta
fuata mchakato ufuatao.
Mafuta yaliyotumiwa ni bidhaa taka yenye madhara na lazima itupwe vizuri. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha usaidizi
au mtoa huduma kwa utupaji/kutumia upya salama kwa bidhaa.
Ondoa Oili
Ni lazima oili imwagwe kutoka kutoka kwenye mrija wa kujazia oili ulio upande wa juu.
1.
Injini ikiwa imezimwa lakini bado ina joto, tenganisha waya wa plagi ya spaki (D,
Kielelezo 15) na uihifadhi mbali na plagi ya spaki (E).
2.
Miundo iliyo na betri iliyowekwa ndani: Tenganisha nyaya (F, Kielelezo 16) na
mota ya kuanzisha.
3.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 17).
4.
Wakati unamwaga oili kutoka kwenye mrija wa kujazia oili wa upande wa juu (C,
Kielelezo 18), weka upande wa injini ulio na plagi ya spaki (E) ukiwa umeangalia
juu. Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
Onyo
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la mafuta
liwe tupu au mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko. Ili kuondoa
mafuta kwenye tangi la fueli, endesha injini hadi isimame kwa kuskosa mafuta.
Ongeza Oili
• Hakikisha injini inadumisha mizani.
• Safisha eneo la kujazia oili kutokana na vifusi vyovyote.
• Tazama Maelezo sehemu ya kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha oili (B, Kielelezo 17) na upanguse
ukitumia kitambaa safi.
2.
Polepole weka oili kwenye eneo la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo 17). Usijaze
kupita kiasi. Baada ya kuongeza oili, subiri dakika moja na kisha ukague kiwango
cha oili.
3.
Weka na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha oili (A, Kielelezo 17).
4.
Ondoa kifaa cha kuangalia oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
ni kuwa juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 17) iliyo kwenye kifaa cha
kuangalia kiwango cha oili.
5.
Weka tena na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha oili (A, Kielelezo 17).
6.
Unganisha waya ya plagi ya spaki (D, Kielelezo 15) kwenye plagi ya spaki (E).
Dumisha Chujio la Hewa
Tazama Kielelezo: 19
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Usiwashe washa na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa
(iwapo kipo) au chujio la hewa (iwapo lipo) vimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu chujio na maji yatayeyusha chujio.
52
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 19).
2.
Ondoa kichujio (C, Kielelezo 19).
3.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo 19), iwapo kipo, kutoka kwenye
kichujio (D). Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio katika eneo gumu.
Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
4.
Osha kisafishaji mwanzo kwa sabuni ya kumimina na maji. Iache ikauke kabisa
kwenye hewa. Usiweke mafuta kwenye kisafishaji cha mwanzo.
5.
Weka pamoja kisafishaji awali kilichokauka, iwapo kipo, kwenye kichujio.
6.
Sakinisha kichujio (C, Kielelezo 19).
7.
Funga kifuniko (B, Kielelezo 19).
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa
moto zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na
kupunguza maisha ya injini.
1.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kuondoa uchafu kutoka kwenye grili ya
kuingiza hewa.
2.
Weka uhusiano, springi na vidhibiti safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, huru kutokana na uchafu
wowote unaoweza kuwaka.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha mafuta, iwapo yapo, yako huru kutokana na
uchafu.
Baada ya kipindi cha muda, uchafu unaweza kukusanyika kwenye mapezi ya
kupoesha silinda na kusababisha injini kuwa moto kushinda kiasi. Uchafu huu hauwezi
kuondolewa bila kutokusanyika kwa kiasi fulani kwa injini. Ruhusu Mtoa Huduma wa
Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa
kama ilivyopendekezwa kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Utupaji wa Kifurushi cha Betri ya
Lithium-Ion
Onyo
Kemikali za betri zina sumu na babuzi.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Mshtuko wa Umeme
• Usiwahi kuchoma au kuharibu kwa kuchoma vifurushi vya betri zilizotupwa
au kutumika kwa kuwa zinaweza kulipuka. Mafusho na nyenzo zenye sumu
zinaundwa vifurushi vya betri vinapochomwa.
• Usitumie betri ambayo imepondwa, kudondoshwa, wala kuharibiwa.
Vifurushi vya betri vilivyotumika na kutupwa bado vinaweza kubeba chaji ndogo
ya umeme na vinapaswa kushughulikiwa kwa uangalifu. Tupa vifurushi vya betri
zilizotumika kwa mujibu wa sheria za shirikisho, jimbo na za ndani.
RBRC (Shirika la Linalotumia Betri Chakavu Inayochajiwa) Nembo
RBRC ni shirika lisilo la faida linalojitolea kutumia betri chakavu
zinazochajiwa. Kupata sehemu ya kukusanya betri chakavu karibu nawe,
piga simu bila malipo kwa 1-800-8-BATTERY au 1-877-2-RECYCLE.
Kwa maelezo zaidi na uorodheshaji wa Maeneo ya Kutumia Betri
chakavu, tembelea RBRC mtandaoni katika www.call2recycle.org.
Hifadhi
BRIGGSandSTRATTON.com