Jinsi ya Kuchaji Betri
Onyo
Hakikisha chaja ya betri ni kavu. Usiweke betri kwenye mvua au unyevunyevu.
1.
Unganisha chaja ya betri (F, Kielelezo 8 9) kwenye plagi ya umeme.
2.
Betri Inayobebeka: Telezesha kifurushi cha betri (G, Kielelezo 8) kwa nguvu
kabisa katika eneo la kuchajia betri (F). Taa nyekundu ya kuchaji isipowaka,
ondoa betri na usakinishe tena. Hakikisha kuwa betri imekaa vyema kabisa katika
eneo la kuchajia betri.
• Taa nyekundu (A, Kielelezo 6) inaashiria betri inachaji kawaida.
• Taa ya kijani (B) inaashiria betri imechajiwa ikajaa.
• Taa nyekundu (C) inayimweka inaashiria betri ni moto sana au baridi sana
na haitakubali chaji. Acha betri ikiwa imeunganishwa na wakati halijoto
ya kawaida ya kuendesha inapofikiwa itaanza kuchaji kiotomati. Tazama
sehemu ya Maelezo ili kujua halijoto ya kawaida ya kuendesha.
• Taa nyekundu/kijani (D) zinazomweka zinaashiria kuwa betri haitachaji na
lazima ibadilishwe.
3.
Betri Inayobebeka: Kutoka "hali tuli", betri itaamka baada ya takriban sekunde
kumi (10).
4.
Betri Inayobebeka: Betri ambayo imeisha nishati kabisa itachaji kikamilifu kwa
takribani saa moja (1). Betri itasalia ina ikiwa imejaa nishati kikamilifu ikiachwa
kwenye chaja.
5.
Betri Inayobebeka: Wakati taa ya kijani inamweka inaashiria kwamba betri
imechajiwa kikamilifu, ondoa betri kwenye chaja.
6.
Betri Iliyowekwa Ndani: Unganisha chaja (G, Kielelezo 9) na injini.
7.
Betri Iliyowekwa Ndani: Betri ambayo imeisha nishati kabisa itachaji kikamilifu
kwa takribani saa nne (4).
8.
Betri Iliyowekwa Ndani: Wakati imeunganishwa na chaja, ikiwa taa zote
zimezima basi betri imejaa nishati. Tenganisha chaja.
9.
Ili kukagua kiwango cha nishati, bonyeza kitufe cha Geji ya Betri (E,
Kielelezo 6 7).
10.
Wakati haitumiki, tenganisha chaja ya betri na plagi ya umeme.
Kipimo cha Fueli ya Betri
Ili kukagua kiwango cha nishati, bonyeza kitufe cha Geji ya Betri (E, Kielelezo 6 7). Taa
za kuonyesha (H) zitaashiria takriban kiwango cha chaji iliyosalia katika betri
Taa za Kuonyesha
Taa nne
Taa tatu
Taa mbili
Taa moja
Taa inamweka
Betri Iliyowekwa Ndani: Wakati imeunganishwa na chaja, ikiwa taa zote zimezima basi
betri imejaa nishati. Tenganisha chaja.
Washa na Uzime Injini
Tazama Kielelezo: 10, 11, 12, 13
Washa Injini
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
Wakati wa Kuwasha Injini
• Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji hewa
(iwapo kipo) vimefungwa na kukazwa.
• Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
• Injini ikifurika, weka choki (ikiwa ipo) katika eneo la kuonyesha FUNGUA au
ENDESHA, songeza kidhibiti injini (ikiwa kipo) hadi eneo la kuonyesha HARAKA
na ushtue hadi injini iwake.
Onyo
Matumizi yasiyofaa ya betri na chaja yanaweza kusababisha mshtuko wa
umeme au moto.
50
Chaji Iliyopo
75% hadi 100%
50% hadi 75%
25% hadi 50%
10% hadi 25%
Chini
Wakati wa Kuendesha Kifaa
• Hakikishachaja ya betri ni kavu (bila unyevunyevu). Usiweke betri kwenye mvua
au unyevunyevu.
• Ili kupunguza hatari ya mshtuko wa umeme, usiruhusu maji yatiririke ndani ya
plagi ya AC.
• Usiweke mkato wa umeme; usiwahi kuweka kifaa chochote katika betri.
Onyo
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi
ya sumu ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika chache. HUWEZI kuiona,
kuinusa wala kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafukizo yanayotolewa,
bado unaweza kupumua gesi ya monoksidi ya kaboni. Iwapo utaanza kuhisi
mgonjwa, kisunzi , au mchovu wakati unatumia bidhaa hii, izime na uende eneo
lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone Daktari. Huenda ukawa umeathiriwa na
sumu ya kaboni monoksidi.
• Tumia bidhaa hii NJE PEKEE mbali na madirisha, milango na matundu ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi kukusanyika na uwezekano wa
kuwa inasambazwa kuelekea maeneo ya nje.
• Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi ya kaboni vinavyotumia
betri pamoja na hifadhi ya betri kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Ving'ora
vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
• USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Gesi ya kaboni monoksidi
inaweza kukusanyika kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa
saa kadhaa, hata baada ya bidhaa hii kuzimwa.
• KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unatelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Kabla ya kuwasha injini,
hakikisha umeongeza oili kulingana na maelekezo yaliyo kwenye mwongozo huu.
Iwapo utawasha injini bila mafuta, itaharibika hadi kushindwa kukarabatiwa na
hutafidiwa chini ya udhamini huu.
Kumbuka: Kifaa kinaweza kuwa na vidhibiti mbali. Tazama mwongozo wa kifaa kwa
utambuzi na uendeshaji wa vidhibiti mbali.
1.
Kagua oili ya injini. Tazama sehemu Kuangalia Kiwango cha Mafuta.
2.
Miundo iliyo na betri inayobebeka: Weka betri (A, Kielelezo 10) katika trei ya
betri juu ya injini. Hakikisha kuwa kifurushi cha betri kimesakinishwa kwa usalama.
Betri inaweza kuwakilisha ufunguo wa kifaa katika hali nyingine.
Kumbuka: Miundo iliyo na betri inayobebeka: Ili kuamsha betri mpya chaji Mara
ya Kwanza ya haraka ya takriban sekunde kumi (10) inahitajika. Tazama sehemu
ya Wakati wa Kuchaji Kifurushi cha Betri .
3.
Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
4.
Songeza kizima mafuta (D, Kielelezo 11), iwapo ipo, hadi eneo la FUNGUA.
5.
Songeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 11), iwapo ipo, hadi eneo la HARAKA.
Endesha injini ikiwa katika eneo la HARAKA.
6.
Miundo iliyo na swichi ya umeme ya kuanzisha: Shikilia wezo wa kusimamisha
injini (C, Kielelezo 12) kwenye sehemu ya kushikia. Songeza swichi ya umeme ya
kuanzisha kwenye sehemu ya ANZA. Tazama mwongozo wa kifaa kwa eneo na
uendeshaji wa swichi ya kuanza ya umeme.
7.
Miundo isiyo na swichi ya umeme ya kuanzisha: Shikilia wezo wa
kusimamisha injini (C, Kielelezo 12) kwenye sehemu ya kushikia. Injini itaanza
kiotomatiki. Tazama mwongozo wa kifaa kwa uendeshaji wa wenzo wa
kusimamisha injini.
Notisi
Ili kurefusha maisha ya kianzishi, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo
wa sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko ya kuanzisha.
Miundo iliyo na betri inayobebeka: Ikiwa injini haitaanza na taa za kuonyesha za
kifurushi cha betri zinamweka, basi betri ni moto sana au umeme unatumika kwa wingi
sana. Taa zote nne za kuonyesha betri (H, Kielelezo 13) zitamweka onyo kwa sekunde
10. Kifurushi cha betri hakina fyuzi, lakini kitawekwa kiotomatiki baada ya sekunde 10.
Ikiwa halijoto ya kifurushi cha betri ni moto sana (zaidi ya 140° F, 60° C), ondoa betri na
uiruhusu kupoa. Ili kuepuka utoaji mwingi wa umeme kwenye mashine ya kukata nyasi,
safisha nyumba ya mashine ili kuondoa nyasi na uchafu.
Kumbuka: Iwapo injini haitaanza baada ya majaribio ya kurudia, wasiliana na muuzaji
aliye karibu nawe au nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au piga simu kwa
1-800-233-3723 (nchini Marekani).
Simamisha Injini
1.
Wenzo wa Kusimamisha Injini: Ondosha wenzo wa kusimamisha injini (E,
Kielelezo 12).
Kidhibiti Injini, ikiwa kina kipengele cha kusimamisha: Songeza kidhibiti injini
(B, Kielelezo 11) hadi eneo la SIMAMA.
BRIGGSandSTRATTON.com