Télécharger Imprimer la page

Briggs & Stratton 090000 Manuel D'utilisation page 47

Masquer les pouces Voir aussi pour 090000:

Publicité

Les langues disponibles
  • FR

Les langues disponibles

  • FRANÇAIS, page 26
• Safirisha tangi la mafuta likiwa TUPU au vali ya kufungia ikiwa katika eneo la
kuonyesha IMEFUNGWA (CLOSED).
Wakati wa Kuhifadhi Mafuta Au Kifaa Kilicho na Mafuta Kwenye Tangi
• Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vitu vingine ambavyo
vina taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto
kwenye mvuke wa mafuta.
Onyo
Kuwasha injini kunatoa cheche.
Cheche zinaweza kuwasha gesi zilizo karibu ambazo zina uwezo wa kuwaka
moto.
Inaweza kusababisha mlipuko na moto.
• Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo, usiwashe injini.
• Usitumie majimaji yaliyoshinikizwa ya kuwasha kwa sababu mvuke unaweza
kuwaka moto.
Onyo
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina monoksidi ya kaboni, gesi
ya sumu ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika chache. HUWEZI kuiona,
kuinusa wala kuionja. Hata kama huwezi kunusa mafukizo yanayotolewa,
bado unaweza kuvuta gesi ya monoksidi ya kaboni. Ukianza kuhisi mgonjwa,
kizunguzungu, au mchovu wakati unatumia bidhaa hii, nenda kwenye eneo
lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa umeathiriwa na
sumu ya kaboni monoksidi.
• Tumia bidhaa hii NJE PEKEE mbali na madirisha, milango na matundu ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi kukusanyika na uwezekano wa
kuwa inasambazwa kuelekea maeneo ya nje.
• Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi ya kaboni vinavyotumia
betri pamoja na hifadhi ya betri kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Ving'ora
vya moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi ya kaboni.
• USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Gesi ya kaboni monoksidi
inaweza kukusanyika kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa
saa nyingi, hata baada ya bidhaa hii kuzimwa.
• KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unatelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
Onyo
Sehemu zinazozunguka zinaweza kugusana au kunasa mikono, miguu, nywele,
nguo, au vifuasi.
Inaweza kusababisha ukataji wa viungo wenye kiwewe au majeraha mabaya ya
ukataji ngozi.
• Endesha kifaa na vilinzi vikiwa karibu.
• Weka mikono na miguu mbali na sehemu zinazozunguka.
• Funga nywele ndefu na uondoe mapambo.
• Usivae nguo zisizokubana vizuri, kamba za nguo zinazomwayamwaya au
vipengee vinavyoweza kushikwa.
Onyo
Injini zinazoguruma zinatoa joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa moto
zaidi.
Unaweza kuchomeka vibaya sana ukiigusa.
Uchafu unaoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi n.k. unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda ya injini na mapezi yapoe kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
• Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442,
kutumia au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa
na brashi, au lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama
ilivyobainishwa katika Sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya
kufanya kazi. Mamlaka mengine ya Majimbo au shirikisho yanaweza kuwa na
sheria sawia. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa kifaa, muuzaji rejareja, au
muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya mfumo wa ekzosi
uliowekwa kwenye injini hii.
Onyo
 Cheche zisizokusudiwa zinaweza kusababisha moto au mrusho wa umeme. 
 Uwashaji usiokusudiwa unaweza kusababisha kunaswa, kukatwa kwa viungo
kwa kiwewe, au majeraha makali ya ukataji wa ngozi. 
 Hatari ya moto 
 Kabla ya kutekeleza marekebisho au ukarabati: 
• Tenganisha waya wa plagi ya spaki na uuweke mbali na plagi ya spaki. 
• Miundo iliyo na betri inayobebeka: Ondoa betri kwenye trei ya betri ya injini.
Betri inaweza kuwakilisha ufunguo wa kifaa katika hali nyingine. 
• Miundo iliyo na betri iliyowekwa ndani: Tenganisha nyaya na mota ya
kuanzisha. 
• Tumia zana sahihi tu. 
• Usihitilafiane na springi ya kidhibiti, viungo, au viungo vingine ili kuongeza kasi ya
injini. 
• Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo
sawa kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zisifanye kazi kwa njia sawa,
zinaweza kuharibu kifaa na inaweza kusababisha majeraha. 
• Usigongegonge gurudumu la kuongeza kasi ya injini kwa nyundo au kifaa kigumu
kwa sababu gurudumu la kuongeza kasi ya injini linaweza kuvunjika wakati wa
kuendesha. 
 Wakati wa kujaribu cheche: 
• Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki. 
• Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa. 
Onyo
 Matumizi yasiyofaa ya betri na chaja yanaweza kusababisha mshtuko wa
umeme au moto. 
 Wakati wa Kuendesha Kifaa 
• Hakikisha chaja ya betri ni kavu. Usiweke betri kwenye mvua au unyevunyevu. 
• Ili kupunguza hatari ya mshtuko wa umeme, usiruhusu maji yatiririke ndani ya
plagi ya AC. 
• Usiweke mkato wa umeme; usiwahi kuweka kifaa chochote katika betri. 
 Unapochaji Betri 
• Chaji betri ya Briggs & Stratton ukitumia chaja ya betri ya Briggs & Stratton
pekee. 
• Usitumie chaja ya betri ya Briggs & Stratton kuchaji betri za aina nyingine yoyote. 
• Hakikisha chaja ya betri ni kavu. Usiweke betri kwenye mvua au unyevunyevu. 
• Ili kupunguza hatari ya uharibifu kwenye plagi ya umeme na kamba, vuta kwa
plagi badala ya kamba wakati wa kutenganisha chaja. 
• Usitumie chaja kwa plagi au kebo iliyoharibika. Kamba ya kusambaza haiwezi
kubadilishwa. Ikiwa kamba imeharibika, chaja inapaswa kubadilishwa mara moja. 
• Usitumie chaja ikiwa imepokea pigo kali, imeangushwa, au vinginevyo kuharibika
kwa njia yoyote. Ikiwa chaja imeharibika ni lazima ibadilishwe. Chaja haiwezi
kufanyiwa huduma. 
• Usitenganishe chaja au kuifanyia huduma. 
• Ili kupunguza hatari ya mshtuko wa umeme, ondoa chaja kwenye plagi kabla ya
kusafisha. 
• Usiweke mkato wa umeme; usiwahi kuweka kifaa chochote katika betri. 
• Chaja haikusudiwi kutumiwa na watu (pamoja na watoto) walio na upungufu
wa uwezo wa kimwili, kihisia au kiakili, au ukosefu wa uzoefu na maarifa,
isipokuwa wawe wamepewa usimamizi au agizo kuhusu matumizi ya kifaa na mtu
anayewajibikia usalama wao. 
• Watoto wanapaswa kusimamiwa ili kuhakikisha kwamba hawachezi na chaja. 
 Kebo ya Kiendelezi 
• Kembo ya kiendelezi haipaswi kutumiwa isipokuwa iwe muhimu kabisa. Matumizi
ya kebo isiyofaa ya kiendelezi yanaweza kusababisha hatari ya moto na mshtuko
wa umeme. Ikiwa lazima kamba ya kiendelezi itumiwe, hakikisha:
1.
Kwamba pini kwenye plagi ya kebo ndefu ni za nambari, ukubwa, na umbo
sawia na plagi iliyo kwenye chaja; 
2.
Kwamba kebo ndefu imewekwa nyaya vizuri na katika hali nzuri ya
kiumeme; na 
3.
Kwamba ukubwa wa waya ni angalau 16 AWG ili kuruhusu ukadiriaji wa
nishati ya AC ya chaja. 
 Wakati wa Kuhifadhi Betri 
47

Publicité

loading

Ce manuel est également adapté pour:

093j00100000