Briggs & Stratton Vanguard 10V000 Manuel D'utilisation page 51

Masquer les pouces Voir aussi pour Vanguard 10V000:
Table des Matières

Publicité

Les langues disponibles
  • FR

Les langues disponibles

  • FRANÇAIS, page 26
Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa imezimwa lakini bado ina joto, tenganisha waya ya plagi ya spaki (D,
Kielelezo 18) na ukiweke mbali na plagi ya spaki (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 19).
3.
Injini ina tundu mbili za kumwaga oili. Ondoa kifuniko kimoja cha tundu la
kumwaga oili (F, H, Kielelezo 20). Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
4.
Baada ya oili kumwagwa, weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F,
H, Kielelezo 20).
Ongeza Oili
• Hakikisha injini inadumisha mizani.
• Safisha eneo la kujazia oili kutokana na vifusi vyovyote.
• Tazama Maelezo sehemu ya kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 19) na upanguse ukitumia
kitambaa safi.
2.
Injini ina matundu mengi ya kujazia oili. Polepole weka oili kwenye tundu
la kujazia oili ya injini (C, G, Kielelezo 20). Usijaze kupita kiasi. Baada ya
kuongeza oili, subiri dakika moja na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Sakinisha kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 19).
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha
oili ni kuwa juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 19) kweny kifaa cha
kupimia kiwango cha mafuta.
5.
Weka tena kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 19).
6.
Unganisha waya ya plagi ya spaki (D, Kielelezo 18) kwenye plagi ya spaki (E).
Badilisha Oili katika Kifaa cha
Upunguzaji
Kifaa cha Upunguzaji Gia kwa Uwiano wa 6:1
Tazama Kielelezo: 21
Iwapo injini yako imewekwa kifaa cha upunguzaji gia kwa uwiano wa 6:1, ifanyie
huduma kama ifuatavyo: 
1.
Ondoa kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 21) na kifuniko cha eno la
kiwango cha oili (B). 
2.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwagia oili (C, Kielelezo 21) na umwage oili
kwenye kontena inayofaa. 
3.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwagia oili (C, Kielelezo 21). 
4.
Ili kujaza, mwaga polepole oili ya kulainisha gia (tazama sehemu ya Maelezo)
kwenye tundu la kujazia oili (D, Kielelezo 21). Endelea kumwaga hadi oili ifurike
kwenye shimo la kiwango cha oili (E). 
5.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kiwango cha oili (B, Kielelezo 21). 
6.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 21). 
Kumbuka: Kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 21) kina shimo ndogo la
kupitishia hewa (F) na ni lazima kiwekwe upande wa juu wa kifuniko cha gia kama
ilivyoonyeshwa. 
Kifaa cha Upunguzaji Gia kwa Uwiano wa 2:1
Tazama Kielelezo: 22 
Ikiwa injini ina kifaa cha upunguzaji nyororo kwa uwiano wa 2:1 (G, Kielelezo 22), basi
hauhitaji kubadilisha oili. Oili katika injini pia inalainisha lifaa cha upunguzaji nyororo. 
Kifaa cha Upunguzaji Klachi Oevu kwa Uwiano wa 2:1
Tazama Kielelezo: 23
Iwapo injini yako imewekwa kifaa cha upunguzaji klachi oevu kwa uwiano wa 2:1, ifanyie
huduma kama ifuatavyo: 
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 23). 
2.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwagia oili (B, Kielelezo 23) na umwage oili
kwenye kontena inayofaa. 
3.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwagia oili (B, Kielelezo 23). 
4.
Ili kujaza, mwaga polepole oili ya kulainisha gia (tazama sehemu ya Maelezo )
kwenye tundu la kujazia oili (C, Kielelezo 23). 
5.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 23). 
6.
Ondoa kifaa cha kupima oili (A, Kielelezo 23) na ukague kiwango cha oili. Kiwango
sahihi cha oili ni kuwa juu ya alama inayoashiria oili imejaa (D) kwenye kifaa cha
kupima kiwango cha oili. 
7.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 23). 
Dumisha Chujio la Hewa
Tazama Kielelezo: 24, 25
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Usiwashe washa na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa
(iwapo kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) vimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu chujio na maji yatayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Chujio la Hewa la Karatasi
1.
Legeza sehemu za kufunga (C, Kielelezo 24).
2.
Ondoa kifuniko (A, Kielelezo 24).
3.
Ondoa chujio (B, Kielelezo 24).
4.
Ili kulegeza uchafu, gongesha chujio (B, Kielelezo 24) kwa utaratibu kwenye
eneo gumu. Ikiwa chujio ni chafu kupita kiasi, badilisha kwa chujio mpya.
5.
Sakinisha chujio (B, Kielelezo 24).
6.
Weka kifuniko (A, Kielelezo 24) na ufunge vizuri kwa sehemu za kufunga (C).
Hakikisha sehemu za kukazia zimekazwa kabisa.
Chujio la Hewa la Karatasi - Nyembamba
1.
Songeza wenzo (A, Kielelezo 25) ili kufungua kifuniko (C).
2.
Songeza sehemu za kufunga (B, Kielelezo 25) ili kuondoa kifuniko (C).
3.
Ondoa chujio (D, Kielelezo 25).
4.
Ili kulegeza vifusi, gongesha chujio (D, Kielelezo 25) kwa utaratibu kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu kupita kiasi, badilisha kwa chujio mpya.
5.
Sakinisha chujio (D, Kielelezo 25).
6.
Sakinisha kifuniko (C, Kielelezo 25). Songeza wenzo (A) hadi eneo la kufunga.
Kumbuka: Kagua jinsi kifuniko cha foam (E, Kielelezo 25) kilivyotoshea. Hakikisha
kwamba kifuniko cha foam nimeingia vizuri mahali pake (F).
Fanyia huduma Mfumo wa Mfuta
Tazama Kielelezo: 26
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto haraka sana na kulipuka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
• Kagua tundu za mafuta, tangi, kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
• Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta , mimina mafuta kutoka kwa
tangi ya mafuta au au funga vali ya kuzuia mafuta.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatavukiza kabla ya kuwasha
injini.
• Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa kwa namna sawa na
sehemu asili.
Chujio Msingi la Mafuta, iwapo lipo
1.
Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 26).
2.
Ondoa chujio msingi la mafuta (B, Kielelezo 26).
3.
Iwapo chujio msingi la mafuta ni chafu, lisafishe au ulibadilishe. Ukibadilisha chujio
msingi la mafuta, hakikisha umetumia chujio msingi la mafuta ambalo si ghushi.
51

Publicité

Table des Matières
loading

Ce manuel est également adapté pour:

Vanguard 12v000

Table des Matières