Ili kuweka kidhibiti injini kwa mbali kwenye mweleko wa kulia, bano la kuweka kebo
((U, Kielelezo 10, nambari ya kipuri 596950) linahitajika. Ili kunua bano la kuweka
kebo, wasiliana na Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa.
1.
Songeza wenzo wa kidhibiti injini / TransportGuard® (A, Kielelezo 6, 10) hadi
eneo la ZIMA.
2.
Ondoa springi (S, Kielelezo 6).
3.
Ondoa sehemu ya kushikia kidhibiti injini (W, Kielelezo 10) ili uone shimo hilo
ndogo (S).
4.
Songeza wenzo wa kidhibiti injini / TransportGuard® (A, Kielelezo 6, 10) hadi
eneo la HARAKA.
5.
Tumia bisibisi ya milimita 10 na ikazue nati (P, Kielelezo 6) geuza nusu
mzunguko kwenye wenzo wa kidhibiti injini / TransportGuard®.
6.
Weka sehemu ya Z ya kebo ya waya gumu (L, Kielelezo 10) kwenye shimo
ndogo (S) lililo katika wenzo wa kidhibiti injini (A).
7.
Ondoa bolti (T, Kielelezo 10). Weka bano la kuweka kebo (U) kwenye eneo
linaloonyeshwa katika Kielelezo 10. Funga bano la kuweka kebo (U) ukitumia
bolti (T). Kaza bolti (T) hadi 30 lb-in (3,4 Nm).
8.
Legeza skrubu (I, Kielelezo 10). Funga vazi la kebo (N) chini ya klampu ya kebo
(M) na ukaze skrubu (I).
9.
Ili kagua utendakazi wa kidhibiti injini kwa mbali, badilisha kasi kwenye kidhibiti
injini kwa mbali kutoka polepole hadi haraka mara kadhaa. Kidhibiti injini kwa
mbali na kebo ya waya gumu (L, Kielelezo 10) zinapaswa kusonga huru. Kaza/
kazua nati (P, Kielelezo 6) kama inavyohitajika ili kuendesha unavyopenda.
Kasi ya Injini Isiyobadilika (Hakuna Kebo ya Kidhibiti Injini)
Tazama Kielelezo: 11, 12
Inapogeuzwa kuwa Kasi ya Injini Isiyobadilika, hakuna kebo ya kidhibiti injini wala
uchaguaji kasi. Haraka ndio kasi pekee ya injini.
1.
Songeza wenzo wa kidhibiti injini / TransportGuard® (A, Kielelezo 11) hadi eneo
la ZIMA.
2.
Ondoa springi (S, Kielelezo 11).
3.
Songeza wenzo wa kidhibiti injini / TransportGuard® (A, Kielelezo 11) hadi eneo
la HASRAKA.
4.
Hakikisha skrubu (V, Kielelezo 11) inapimana na shimo katika bano. Kaza skrubu
(V) hadi 25 lb-in (2,8 Nm).
5.
Ondoa kiungo cha kidhibiti (H, Kielelezo 11).
Kumbuka: Wenzo wa kidhibiti injini / TransportGuard® sasa utakuwa na maeneo
mawili pekee: Eneo la kuonyesha SIMAMA / ZIMA na eneo la kuonyesha ENDESHA.
6.
Weka lebo mpya ya TransportGuard® ya WASHA / ZIMA (O, Kielelezo 12) juu ya
lebo iliyopo ya udhibiti kasi iliyo kwenye paneli ya kando (F).
Uendeshaji
Mapendekezo ya Oili
Kiwango cha Oili: Tazama sehenmu ya Vipimo.
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza mafuta kwenyeinjini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya
kwanza, hakikisha umekagua kiwango cha oili na uongeze oili kulingana na maagizo
kwenye mwongozo huu. Iwapo utawasha injini bila mafuta, itaharibika hadi kushindwa
kukarabatiwa na hutafidiwa chini ya udhamini huu.
Tunapendekeza matumizi ya oili Zilizoidhinishwa na Hakikisho la Briggs & Stratton
kupata utendakazi bora. Oili nyingine za usafishaji zinakubalika ikiwa zimebainishwa
kwa huduma ya SF, SG, SH, SJ au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum.
Hali joto ya nje inabainisha mnato sahihi wa oili kwa injini. Tumia chati kuchagua mnato
bora zaidi kwa hali joto ya nje inayotarajiwa. Injini katika vifaa vingi vya nje zinafanya
kazi vyema zikitumia oili ya 5W-30 Synthetic. Kwa vifaa vinavyoendeshwa katika joto la
®
juu, oili ya Vanguard
15W-50 Synthetic inatoa ulindaji bora.
48
A
SAE 30 - Chini ya 40 °F (4 °C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa
kuwasha.
B
10W-30 - Juu ya 80 °F (27 °C) matumizi ya 10W-30 yanaweza kusababisha
ongezeko la matumizi ya oili. Kagua kiwango cha oili mara nyingi zaidi.
C
5W-30
Sinthetiki 5W-30
D
E
®
Vanguard
Synthetic 15W-50
Kagua Kiwango cha Oili
Tazama Kielelezo: 13, 14
Kabla ya kuongeza au kukagua oili
• Hakikisha injini inadumisha mizani.
• Safisha eneo la kujazia oili kutokana na vifusi vyovyote.
• Tazama Maelezo sehemu ya uwezo wa mafuta.
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila mafuta. Watengenezaji au
wauzaji vifaa huenda waliongeza mafuta kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa
mara ya kwanza, hakikisha umekagua kiwango cha oili na uongeze oili kulingana na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, itaharibika kiasi kwamba
haiwezi kukarabatiwa na hautafidiwa chini ya udhamini.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 13) na upanguse ukitumia
kitambaa safi.
2.
Sakinisha kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 13).
3.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili ni
kuwa juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 13) kweny kifaa cha kupimia
kiwango cha mafuta.
4.
Injini ina matundu mengi ya kujazia oili (C, G, Kielelezo 14). Iwapo kiwango cha
oili kiko chini, ongeza oili polepole kwenye tundu moja la kujazia ooili ya injini (C,
G). Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza oili, subiri dakika moja na kisha
ukague kiwango cha oili.
5.
Weka tena kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 13).
Mfumo wa Ulinzi wa Chini wa Mafuta
(iwapo upo)
Baadhi ya modeli zina kihisio cha mafuta ya chini. Iwapo mafuta yako chini, kihisio aidha
kitaamilisha mwangaza wa tahadhari au kusimamisha injini. Simamisha injini na ufuate
®
ili
hatua hizi kabla ya kuwasha tena injini.
• Hakikisha injini iko katika sehemu laini.
• Angalia kiwango cha mafuta. Tazama sehemu Kuangalia Kiwango cha Mafuta.
• Iwapo kiwango cha mafuta kiko chini, ongeza kiwango sahihi cha mafuta. Washa
injini na uhakikishe mwangaza wa tahadhari (iwapo upo) haujaamilishwa.
• Iwapo kiwango cha mafuta hakiko chini, usiwashe injini. Wasiliana na Mtoa
Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa ili kurekebisha matatizo ya mafuta.
Mapendekezo ya Mafuta
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
• Petroli safi, freshi, isiyo na risasi (unleaded).
• Kiwango cha chini zaidi cha okteni 87/AKI 87 (91 RON). Matumizi katika mwinuko
wa juu, tazama hapa chini.
• Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasoholi) inakubalika.
Notisi
Usitumie petroli ambayo haijaidhinishwa, kama vile E15 na E85.
Usichanganye oili kwenye petroli au kurekebisha injini ili itumie mafuta mbadala.
Utumizi wa mafuta ambayo hayajaidhinishwa utaharibu vipengele vya injini, jambo
ambalo halijasimamiwa na hakikisho.
VanguardPower.com