Briggs & Stratton 190000 Manuel D'utilisation page 45

Table des Matières

Publicité

Les langues disponibles
  • FR

Les langues disponibles

  • FRANÇAIS, page 22
 Masharti Wastani ya Udhamini 
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 3
 1 
 
 Haya ni masharti yetu wastani ya hakikisho, lakini mara kwa mara huenda
kukawa na vipengele vya ziada vinavyosimamiwa na hakikisho ambavyo
havikusimamiwa wakati wa uchapishaji. Ili kupata orodha ya masharti ya sasa
ya hakikisho la injini yako, nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au
uwasiliane na Muuzaji Huduma wako Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton. 
 2 
 
 Hakuna hakikisho kwa injini za vifaa vilivyotumiwa kutoa nishati badala ya kifaa
kinachofaa; jenereta ya akiba kwa madhumuni ya kibiashara, magari ya kubebea
mizigo yanayozidi 25 MPH, au injini zinazotumiwa katika mashindano ya mbio au
kwenye viwanja vya kibiashara au vya kukodishwa. 
 3 
 
 Vanguard iliyowekwa kwenye jenereta ya akiba: miezi 24 kwa matumizi ya
kibinafsi, hakuna hakikisho kwa matumizi ya kibinafsi. Msururu wa Kibiashara ulio
na tarehe ya kutengenezwa ya kabla ya Julai 2017, miezi 24 kwa matumizi ya
kibinafsi, miezi 24 kwa matumizi ya kibiashara. 
 4 
 
 Nchini Australia - Bidhaa zetu huja na hakikisho ambalo haziwezi
kutojumuishwa chini ya Sheria ya Mtumiaji ya Australia. Una haki ya kubadilishiwa
au kurudishiwa pesa kwa hitilafu kuu au fidia kwa uharibifu au hasara nyingine
yoyote ya siku za usoni. Pia una haki ya bidhaa kufanyiwa ukarabati au
kubadilishwa endapo bidhaa hazitakuwa za ubora unaokubaliwa na hitilafu
haimaanishi kuharibika kwa njia kubwa. Ili kupata huduma ya hakikisho, tafuta
Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe kwenye ramani
yetu ya kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM, au kwa
kupiga simu kwa nambari 1300 274 447, au kwa kutuma barua pepe kwa
salesenquiries@briggsandstratton.com.au, au kutuma barua kwa Briggs &
Stratton Australia Pty Ltd, 1 Moorebank Avenue, Moorebank, NSW, Australia,
2170. 
Kipindi cha hakikisho kinaanzia tarehe ya ununuzi wa mtumiaji wa kwanza wa rejareja
au wa kibiashara. "Matumizi ya kibinafsi" inamaanisha matumizi ya kibinafsi ya
nyumbani ya mtumiaji wa rejareja. "Matumizi ya kibiashara" inamaanisha matumizi
mengine yote, yakijumuisha matumizi kwa madhumuni ya kibiashara, ya kuzalisha
mapato au ya kukodisha. Pindi tu injini inapopitia matumizi ya kibiashara, baada ya
hapo itazingatiwa kuwa injini ya matumizi ya kibiashara kwa ajili ya hakikisho hili. 
Hifadhi risiti yako ya ushahidi wa ununuzi. Ukikosa kutoa ushahidi wa tarehe
ya kwanza ya ununuzi wakati huduma ya hakikisho inapoombwa, tarehe ya
utengenezaji wa bidhaa itatumiwa kung'amua kipindi cha hakikisho. Usajili
wa bidhaa hauhitajiki ili kupata huduma ya hakikisho kwa bidhaa za Briggs &
Stratton. 
Kuhusu Hakikisho Lako 
Hakikisho hili lenye kipimo linasimamia tu nyenzo zinazohusiana na injini na/au
utendakazi, na sio kubadilishiwa au kurudishiwa pesa ulizonunua kifaa ambacho kina
injini husika. Udumishaji, uimarishaji, marekebisho ya mara kwa mara au kuchakaa
na kuchanika kwa kawaida hazijasimamiwa na hakikisho hili. Vile vile, hakikisho
halitumiki ikiwa injini imehitilafiwa au kubadilishwa au ikiwa nambari tambulishi ya
injini imeharibiwa ua kuondolewa. Hakikisho hili halisimamii uharibifu kwenye injini au
matatizo ya utendakazi wa injini yanayosababishwa na: 
1.
Matumizi ya sehemu ambazo si sehemu halisi za Briggs & Stratton; 
2.
Kuendesha injini zilizo na oili isiyotosha, chafu, au ya ubora usio sahihi; 
3.
Matumizi ya mafuta machafu au yaliyoharibika, petroli yaliyotengenezwa kwa zaidi
ya 10% ya ethanoli, au matumizi ya mafuta kama vile petroli iliyoevuka au gesi
asili kwenye injini ambazo hazijaundwa/kutengenezwa tangu mwanzo na Briggs &
Stratton kuendeshwa kwa mafuta kama hayo; 
4.
Uchafu ulioingia kwenye injini kwa sababu ya udumishaji kwa kutumia kisafishaji
hewa kisichofaa au ufunganishaji mbaya; 
5.
Kugonga kitu kwa visu vya kukata vya mashine ya kukatia nyasi, adapta, impela
au vifaa vingine vya shafti kombo ambavyo vimelegea au havijawekwa ifaavyo au
ukazaji wa v-belt kupita kiasi; 
6.
Sehemu au vifaa vinavyohusiana kama vile klachi, gia, vidhibiti vya kifaa, nk.,
ambavyo havijatolewa na Briggs & Stratton; 
7.
Joto kupita kiasi kutokana na vipande vya nyasi, uchafu na vifusi, au viota vya
panya vinavyoziba au kufunika vifaa vya kupoesha au eneo la gurudumu la
kuongeza kasi, au kuendesha injini bila uingizaji hewa wa kutosha; 
8.
Mtetemo kupita kiasi kwa ajili ya kasi kupita kiasi, uwekaji injini ikilegea, visua
kukata au impele ambazo zimelegea au havijasawazishwa, au uunganishaji
vibaya wa vipengele vya vifaa kwenye shafti kombo; 
9.
Matumizi mabaya, ukosefu wa udumishaji wa mara kwa mara, usafirishaji,
ushughulikiaji, au uwekaji injini vibaya. 
Huduma ya hakikisho inapatikana tu kupitia Wauzaji Huduma Walioidhinishwa wa
Briggs & Stratton. Tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe
kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au
kwa kupiga simu kwa nambari 1-800-233-3723 (nchini Marekani). 
80004537 (Rev. F) 
1, 2, 3
  
45

Publicité

Table des Matières
loading

Ce manuel est également adapté pour:

250000

Table des Matières