Briggs & Stratton 190000 Manuel D'utilisation page 43

Table des Matières

Publicité

Les langues disponibles
  • FR

Les langues disponibles

  • FRANÇAIS, page 22
Ongeza Mafuta
• Hakikisha kuwa mtambo uko katika kiwango.
• Safisha eneo la kujaza mafuta kutokana na uchafu wowote.
• Tazama Vipimo katika eneo la kiwango cha mafuta.
Kifuniko cha Fueli, iwapo kipo
1.
Ondoa kifuniko cha fueli (H, Kielelezo 10).
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la mtambo (C, Kielelezo
10). Jaza hadi sehemu ya kufurika.
3.
Sakinisha na ukaze kifuniko cha fueli (H, Kielelezo 10).
4.
Unganisha waya wa kuziba cheche (D, Kielezo 9) kwenye kuziba cheche (E).
Kifaa Kifupi cha Kuangalia Mafuta, iwapo kipo
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 10) na upanguse
kwa kitambaa safi.
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la injini (C, Kielelezo 10).
Jaza hadi sehemu ya kufurika.
3.
Sakinisha kifaa cha kupima mafuta (A, Kielelezo 10). Usigeuze au kukaza.
Ondoa na uangalie kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha mafuta kiko juu ya
kiashiria kilichojaa (B) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta.
4.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo
10).
5.
Unganisha waya ya kuziba cheche kwenye kuziba cheche (E) (D, Figure 9).
Kifaa kipana cha kuangalia mafuta, iwapo kipo
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia mafuta (A, Kielelezo 11) na ukipanguse kwa kitambaa
safi.
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la injini (C, Kielelezo 11).
Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza mafuta, subiri dakika moja (1) na kisha
angalia kiwango cha mafuta.
3.
Sakinisha na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 11).
4.
Ondoa na uangalie kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha mafuta kiko juu ya
kiashiria kilichojaa kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (B, Kielelezo
11) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta.
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo
11).
6.
Unganisha waya ya kuziba cheche kwenye kuziba cheche (E) (D, Figure 9).
Shughulikia Kichuja Hewa
Tazama Kelelezo: 12, 13, 14
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
• Kamwe usiwashe na kuendesha wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo
kipo) au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Modeli mbalimbali aidha zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia
zinaweza kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na
kutumiwa tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye
injini yako na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 12) inayoshikilia kifuniko (B).
2.
Ondoa kifuniko cha (B, Kielelezo 12) na kichujio kichujio (D).
3.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio (D, Kielelezo 12) katika eneo
gumu. Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
4.
Sakinisha kichujio (D, Kielelezo, 12).
5.
Sakinisha kifuko na ukilinde kwa bizimu (A), (B, Kielelezo 12). Hakikisha bizimu
zimekazwa.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 13) na uondoe kifuniko (B).
2.
Ondoa bizimu (C, Kielelezo 13) na kichujio (D).
3.
Ondoa kichujio cha mwanzo (E, Kielelezo 13), iwapo kipo, kutoka kwenye kichujio
(D).
4.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio (D, Kielelezo 13) katika eneo
gumu. Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
5.
Osha kisafishaji cha mwanzo (E, Kielelezo 13) kwenye sabuni oevu na maji.
Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta kwenye
kisafishaji cha mwanzo.
6.
Kusanya kisafishaji cha mwanzo kilichokauka (E, Kielelezo 13) kwenye kichujio
(D).
7.
Sakinisha kisafishaji muhuri (F, Kielelezo 13), kichujio (D), na kisafishaji cha
mwanzo (E), kwenye eneo la kichujio cha hewa (G) na kwenye kitufe (H).
Hakikisha kichujio kimeunganishwa sahihi kwenye eneo na kulinda kwa bizimu
(C).
8.
Sakinisha kifuko na ukilinde kwa bizimu (A), (B, Kielelezo 13). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Kichujio cha Povu ya Hewa
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 14) inayoshikilia kifuniko (B).
2.
Fungua funiko (B, Kielelezo 14) na uondoe kichujio (C).
3.
Osha kipengele cha povu (C, Kielelezo 14) kwenye sabuni oevu na maji. Finyiza ili
kukausha kipengele cha fomu kwenye kitambaa safi.
4.
Koleza kipengele cha povu (C, Kielelezo 14) kwa mafuta safi ya injini. Ili kuondoa
mafuta ya kupita kiasi ya injini, finyiza kipengele cha povu kwenye kitambaa safi.
5.
Sakinisha kichujio (C, Kielelezo 14).
6.
Sakinisha jalada (B, Kielelezo 14) na ulinde kwa bizimu(s) (A).
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa
moto zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na
kupunguza maisha ya injini.
1.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kuondoa uchafu kutoka kwenye grili ya
kuingiza hewa.
2.
Weka uhusiano, springi na vidhibiti safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, huru kutokana na uchafu
wowote unaoweza kuwaka.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha mafuta, iwapo yapo, yako huru kutokana na
uchafu.
Baada ya kipindi cha muda, uchafu unaweza kukusanyika kwenye mapezi ya
kupoesha silinda na kusababisha injini kuwa moto kushinda kiasi. Uchafu huu hauwezi
kuondolewa bila kutokusanyika kwa kiasi fulani kwa injini. Ruhusu Mtoa Huduma wa
Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa
kama ilivyopendekezwa kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuhifadhi Mafuta Au Kifaa Kilicho na Mafuta Kwenye Tangi
• Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vitu vingine ambavyo
vina taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto
kwenye mvuke wa mafuta.
Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 15 
43

Publicité

Table des Matières
loading

Ce manuel est également adapté pour:

250000

Table des Matières