Briggs & Stratton 110000 Manuel D'utilisation page 51

Table des Matières

Publicité

Les langues disponibles
  • FR

Les langues disponibles

  • FRANÇAIS, page 31
Washa Injini
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza
kuachilia. Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo
kuteguka.
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Unapowasha injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji
hewa (iwapo kipo) vimefungwa vizuri.
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
Ikiwa injini imefurika, choki (iwapo ipo) imewekwa kwenye eneo la
IMEFUNGULIWA au ENDESHA. Songeza kidhibiti injini (iwapo kipo) hadi
kwenye eneo la HARAKA na ushtue hadi injini iwake.
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
ONYO 
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu.
Ili kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na
mbali na madirisha, milango na matundu.
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia
betri pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya
mtengenezaji. Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni
monoksidi.
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
NOTISI 
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza oili kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha oili ni sahihi. Ongeza oili kama ilivyobainishwa na
maagizo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha injini bila oili, injini itaharibika na haiwezi
kukarabatiwa chini ya waranti.
Aina za Mfumo wa Kuwasha
Kabla ya kuwasha injini, ni lazima ujue aina ya mfumo wa kuwasha ambao uko kwenye
injini yako. Injini yako ina mojawapo ya aina hizi.
®
ReadyStart
na Mfumo wa Kuwasha kwa Hatua-1: Mifumo hii ina choki
otomatiki inayodhibitiwa na halijoto. Haina choki ya kudhibiti mwenyewe wala
prima.
Mfumo wa Choki: Mfumo huu una choki ya kutumiwa katika halijoto baridi.
Haina prima.
Ili kuwasha injini yako, fuata maelekezo ya aina yako ya mfumo wa kuwasha.
KUMBUKA: Kifaa chako kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Rejelea mwongozo wa
kifaa ili utambue mahali ambapo vidhibiti vya mbali viko na jinsi ya kuvitumia.
®
ReadyStart
na Mfumo wa Kuwasha kwa Hatua-1
1.
Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
2.
Hakikisha kwamba vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Sogeza kizima mafuta (A, Kielelezo 8), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
FUNGUA.
4.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 8, 9), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo linaloonyesha HARAKA.
5.
Sukuma swichi ya kuzima (D, Kielelezo 8, 9), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
WASHA.
6.
Shikilia wenzo wa kuzima injini (C, Kielelezo 10), iwapo upo, dhidi ya kishikilio.
7.
Kianzishaji cha Kamba, iwapo kipo: Kwa uthabiti shikilia kishikilio cha kamba
ya kianzishaji (E, Kielelezo 8, 9). Vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi
upinzani, kisha vuta haraka.
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta
mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Inaweza kupelekea
mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka
wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na
kisha uvute haraka.
8.
Kianzishaji cha Umeme, iwapo kipo: Geuza swichi ya kianzishaji cha umeme
hadi eneo linaloonyesha WASHA/ANZA.
NOTISI 
Ili kurefusha maisha ya kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo wa
sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko ya kuanzisha.
KUMBUKA: Injini ikikosa kuwasha, wasiliana na muuzaji wako wa ndani au nenda
kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au upige simu kwa nambari 1-800-444-7774
(nchini Marekani).
Mfumo wa Choki
1.
Kagua oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili.
2.
Hakikisha kwamba vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Sogeza kizima mafuta (A, Kielelezo 8), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
FUNGUA.
4.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 8, 9), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
HARAKA. Endesha injini ikiwa katika eneo linaloonyesha HARAKA.
5.
Sogeza kidhibiti choki (F, Kieleleza 8), hadi eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
KUMBUKA: Kwa kawaida choki haihitajiki wakati wa kuwasha upya injini iliyochemka.
6.
Shikilia wenzo wa kusimamisha injini (C, Kielelezo 10) dhidi ya kishikilio.
7.
Kianzishaji cha Kamba, iwapo kipo: Kwa uthabiti shikilia kishikilio cha kamba
ya kianzishaji (E, Kielelezo 8, 9). Vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi
upinzani, kisha vuta haraka.
ONYO 
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta
mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Inaweza kupelekea
mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka
wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na
kisha uvute haraka.
8.
Kianzishaji cha Umeme, iwapo kipo: Geuza swichi ya kianzishaji cha umeme
hadi eneo linaloonyesha WASHA/ANZA.
NOTISI 
Ili kurefusha maisha ya kianzishaji, tumia misururu mifupi ya kuanzisha (upeo wa
sekunde tano). Subiri dakika moja kati ya mizunguko ya kuanzisha.
9.
Injini inapochemka, sogeza kidhibiti choki (F, Kilelelezo 8) hadi eneo linaloonyesha
FUNGUA / ENDESHA.
KUMBUKA: Injini ikikosa kuwasha, wasiliana na muuzaji wako wa ndani au nenda
kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au upige simu kwa nambari 1-800-444-7774
(nchini Marekani).
Zima Injini
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Usikabe kabureta (iwapo ipo) ili kusimamisha injini.
1.
Wenzo wa Kuzima Ijini, iwapo upo: Achilia wenzo wa kuzima injini (E, Kielelezo
10).
2.
Swichi ya Kuzima, iwapo ipo: Sogeza swichi ya kuzima (D, Kielelezo 8, 9) hadi
eneo linaloonyesha ZIMA.
3.
Kidhibiti Injini, iwapo kipo: Songeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 8, 9) hadi eneo
linaloonyesha SIMAMA.
4.
Ufunguo wa Kianzishaji kwa Umeme, iwapo upo Geuza ufunguo wa kianzishaji
kwa umeme hadi eneo linaloonyesha ZIMA / SIMAMISHA. Ondoa ufunguo na
uuweke katika mahali salama mbali na watoto.
51

Publicité

Table des Matières
loading

Ce manuel est également adapté pour:

120000123p00

Table des Matières