•
Tumia kijaribio cha kuziba cheche kilichoidhinishwa.
•
Usikague cheche na kiziba cheche imeondolewa.
Vipengele na Vidhibiti
Vidhibiti vya Mtambo
Linganisha mfano (Kielelezo: 1, 2) na injini yako ili kujifahamisha na eneo la vipengele na
vidhibiti mbalimbali.
A.
Nambari Tambulishi za Injini Modeli - Aina - Msimbo
B.
Kiziba Cheche
C.
Kisafishaji cha Hewa
D.
Kifaa cha Kupima mafuta
E.
Kuziba ya Kumwaga Mafuta
F.
Grili ya Kuingiza Hewa
G.
Kichuja Hewa
H.
Kianzishi cha Umeme
I.
Kabureta
J.
Kichujio cha Fueli (iwapo kipo)
K.
Pampu ya Fueli (iwapo ipo)
L.
Kitoaji Mafuta cha Haraka (iwapo kipo)
M.
Kipozaji cha Fueli (iwapo kipo)
N.
Kitengo cha Kudhibiti Umeme (iwapo kipo)
Ishara za Kudhibiti Injini na Maana
Ishara
Maana
Kasi ya injini - HARAKA
Kasi ya injini - SIMAMA
Kuwasha injini - Choki
IMEFUNGWA
Kifuniko cha Mafuta
Kizima fueli -
KILICHOFUNGULIWA
Kiwango cha mafuta - Upeo
Usijaze kupita kiasi
Oparesheni
Mapendekezo ya Mafuta
Kiwango cha Mafuta: Tazama Vipimo Maalum sehemu.
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila mafuta. Watengenezaji au wauzaji vifaa
huenda waliongeza mafuta kwenye injini. Kabla ya kuwasha injini kwa mara ya kwanza,
hakikisha umekagua kiwango cha mafuta na umeongeza mafuta kulingana na maagizo
kwenye mwongozo huu. Iwapo utawasha injini bila mafuta, itaharibika hadi kushindwa
kukarabatiwa na hutafidiwa chini ya udhamini huu.
46
Ishara
Maana
Kasi ya injini - POLEPOLE
WASHA - ZIMA
Kuwasha injini - Choki
IMEFUNGULIWA
Kizima fueli -
KILICHOFUNGWA
Tunapendekeza matumizi ya mafuta Yaliyoidhinishwa na Udhamini wa Briggs & Stratton
kwa utendakazi bora. Mafuta mengine yaliyo na sabuni ya kiwango cha juu yanakubalika
iwapo yamebainishwa kwa huduma ya SF, SG, SH, SJ au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi
maalum.
Halijoto ya nje inatambua mnato sahihi wa mafuta wa injini. Tumia chati kuteua mnato
bora wa masafa ya halijoto ya nje inayotarajiwa. Injini katika vifaa vingi vya nje huendeshwa
vizuri na mafuta ya Kisinthetiki ya 5W-30. Kwa vifaa vinavyoendeshwa katika halijoto ,
mafuta ya Kisinthetiki ya Vanguard™ 15W-50 hutoa ulinzi bora zaidi.
A
SAE 30 - Chini ya 40 °F (4 °C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa
kuwaka.
B
10W-30 - Juu ya 80 °F (27 °C) matumizi ya 10W-30 yanaweza kusababisha
uongezekaji wa matumizi ya mafuta. Angalia kiwango cha mafuta mara kwa mara.
C
5W-30
D
Sinthetiki 5W-30
E
Vanguard™ Synthetic 15W-50
Angalia Kiwango cha Mafuta
Tazama Kelelezo: 3
Kabla ya kuongeza au kuangalia mafuta
•
Hakikisha kuwa mtambo uko katika kiwango.
•
Safisha eneo la kujaza mafuta kutokana na uchafu wowote.
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 3) na upanguse kwa
kitambaa safi.
2.
Sakinisha na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 3).
3.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta na ukague kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha
mafuta kiko juu ya kiashiria kilichojaa (B, Kielelezo 3) kwenye kifaa cha kuangalia
kiwango cha mafuta.
4.
Iwapo kiwango cha mafuta kiko chini, kwa utaratibu ongeza mafuta kwenye eneo la
mafuta (C, Kielelezo 3). Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza mafuta, subiri
dakika moja na kisha angalia kiwango cha mafuta.
Kumbuka: Usiongeze mafuta kwenye kitoaji mafuta cha haraka, (D, Kielelezo 3), iwapo
kipo.
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 3).
Mfumo wa Ulinzi wa Chini wa Mafuta
(iwapo upo)
Baadhi ya modeli zina kihisio cha mafuta ya chini. Iwapo mafuta yako chini, kihisio aidha
kitaamilisha mwangaza wa tahadhari au kusimamisha injini. Simamisha injini na ufuate
hatua hizi kabla ya kuwasha tena injini.
•
Hakikisha injini iko katika sehemu laini.
•
Angalia kiwango cha mafuta. Tazama sehemu Kuangalia Kiwango cha Mafuta.
•
Iwapo kiwango cha mafuta kiko chini, ongeza kiwango sahihi cha mafuta. Washa
injini na uhakikishe mwangaza wa tahadhari (iwapo upo) haujaamilishwa.
•
Iwapo kiwango cha mafuta hakiko chini, usiwashe injini. Wasiliana na Mtoa Huduma
wa Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa ili kurekebisha matatizo ya mafuta.
Mapendekezo ya Fueli
Lazima fueli ikithi mahitaji haya:
BRIGGSandSTRATTON.com