9. Ukarabati na Uhifadhi
Ili udumishe uwezo wa mashine kufanya kazi salama na kwa
ufanisi, ni muhimu sana ufuate maelekezo yafuatayo kwa ajili
ya ukarabati na uhifadhi.
!
ONYO! Kabla ya kufanya ukarabati au usafishaji
wowote, zima injini na usubiri hadi ubapa wa mashine
usimame kabisa. Ondoa buti ya spaki plagi kutoka kwa spaki
plagi.
9.1 Maelezo Kawaida ya Ukarabati
1. Kaza nati zote, komeo na parafujo ili uwe na uhakika
kwamba kifaa iko katika hali salama ya kufanya kazi.
2. Angalia kifaa kinachoshikilia nyasi mara nyingi ili ukague
uchakavu au kuzorota.
3. Badilisha sehemu chakavu au zilizoharibika kwa ajili ya
usalama.
4. Ukarabati usiofaa, matumizi ya vipengele ambavyo
havijadhibitishwa au bandia, au kuondoa au kubadilisha
vipengele vya usalama inaweza kuharibu mashine na
kuwadhuru waendeshaji sana.
5. Tumia ubapa na sehemu zingine za vipuri zilizopendekezwa
na Briggs & Stratton. Matumizi ya sehemu zisizo halali
inaweza kuharibu mashine na kuwadhuru waendeshaji. Weka
mashine katika hali nzuri ya kufanya kazi..
9.2 Kupindua Mashine
Kwa ajili ya usafishaji au ukarabati wowote ambao unahusu
upande wa chini wa deki, fuata utaratibu huu kupendua
mashine ili ufikie eneo hili la mashine:
1. Mwaga mafuta kutoka kwa tenki; wacha injini ikinguruma
hadi petroli iishe:
• Usiwahi kuwacha mashine ikinguruma bila wewe kuwa
hapo karibu.
• Tumia tu katika eneo iliyo na usambazaji wa hewa vizuri.
• Ikiwa tanki la mafuta lazima likaushwe, litapaswa
kukaushwa nje ya nyumba.
2. Pendusha mashine kando:
• Daima pendusha na upande wa kifaa cha kupunguza
sauti ya eksozi kikiangalia sakafu.
• Usipendushe kwa digrii zaidi ya 90.
9.3 Kuosha
Mashine inapaswa kusafishwa kabisa baada ya kila matumizi.
Daima safisha mashine baada ya matumizi;
• Usiruhusu nyasi uchafu na uchafu mwingine kuwa kavu
na ngumu juu ya sehemu yoyote ya mashine.
• Nyasi kavu na uchafu unaweza kudhibiti operesheni ya
mashine.
Nyasi na uchafu mkavu unaweza kuwa ngumu zaidi
kuondoa bila uharibifu wa mashine.
9.3.1 Jinsi ya Kuosha
Kwa kutoa chaji kutoka kando na kwa modeli za
kukusanya
Safisha uchafu wote wa nyasi kutoka kifaa cha kutolea
uchafu(ya kando na/au ya nyuma).
Kwa modeli zingine zote
Fuata utaratibu hapo juu katika kifungu cha 9.2 Kupindua
Mashine.
Safisha sehemu ya chini ya deki kabisa.
14
9.4 Usafishaji na Ukarabati wa Injini
!
KUMBUKA! Rejelea Mwongozo wa Opereta wa injini
kwa ukarabati wa injini.
!
KUMBUKA! Kagua na/au ubadilishe breki pedi za injini
katika kituo cha huduma mara kwa mara, sehemu za
kiasili tu ndio zinatumika kama vipuri.
9.5 Utaratibu wa Ubapa
!
ONYO! Kabla ya kufanya ukarabati au usafishaji
wowote, zima injini na usubiri hadi ubapa wa mashine
usimame kabisa. Ondoa buti ya spaki plagi kutoka kwa spaki
plagi.
• Ili ukagua muunganisho wa ubapa, Fuata utaratibu hapo
juu katika kifungu cha 9.2 Kupindua Mashine.
• Kagua ubapa mara kwa mara (B katika Kielelezo.37)
kwa ajili ya uchakavu au uharibifu pamoja na kuvunjika,
kukunjika, kuumbua na kadhalika. Hakikisha kuwa makali
ya ubapa yako sawa(Ubapa butu hautakata nyasi, ila
yatageuza ncha ya nyasi kwa rangi ya udongo).
• Kagua komeo (D katika Kielelezo.37) inayoshikilia
ubapa kwa nafasi yake mara kwa mara; Hakikisha komeo
imekazwa.
• Kama ubapa umegonga kitu, , zima injini mara moja,
tenganisha buti ya spaki plagi kutoka kwa spaki plagi.
Kagua muunganisho wote wa ubapa ambayo inajumuisha
komeo(D katika Kielelezo.37), inayoosha(C katika
Kielelezo.37), Ubapa (B katika Kielelezo.37) na adapta ya
ubapa (A katika Kielelezo.37).
• Kama sehemu yoyote ya muunganisho wa ubapa
imeharibika, inafaa kubadilishwa mara moja. Usiwahi
tumia mashine hii ikiwa na sehemu ilivyoharibika.
• Muunganisho wa ubapa unafaa kubadilishwa angalau
kwa kila miaka miwili ya matumizi.
• Wakati unabadilisha sehemu yoyote ya muunganisho wa
ubapa, sehemu zingine zote za muunganisho wa ubapa
zinapaswa kubadilishwa kwa wakati mmoja.
!
KUMBUKA! Muunganisho wa ubapa unafaa
kuondolewa na kuhudumiwa na ajenti aliyethibitishwa
wa Briggs & Stratton.
!
KUMBUKA! Tumia sehemu asili na zilizopendekezwa
pekee za Briggs & Stratton. Sehemu zingine zozote
zinaweza kuwa hazifai na zinaweza kuhatarisha usalama.
• Wakati unafunganisha sehemu za ubapa, nguvu ya
komeo ya ubapa inafaa kuwa kati ya 45nm na 55Nm.
Kielelezo 37
.
www.murray.com