Shughulikia Mfumo wa Eneo la kutolea
moshi
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa moto
zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi n.k. unaweza kushika
moto.
•
Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
•
Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
•
Ni ukiukaji wa Msimbo wa Rasilimali wa Umma wa California, Sehemu ya 4442,
kutumia au kuendesha injini katika eneo linazungukwa na msitu, lililozungukwa na
brashi, au lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa eneo la kutolea moshi una kishika
cheche, kama ilivyofafanuliwa kwenye Sehemu ya 4442, iliyodumishwa kwenye
mpangilio wenye ufanisi wa kufanya kazi. Mamlaka mengine ya Majimbo au shirikisho
yanaweza kuwa sheria sawa. Wasiliana na mtengenezaji wa kifaa asili, muuzaji wa
rejareja, au mtoa huduma ili kupata kishika cheche kilichobuniwa kwa mfumo wa
eneo la kutolea moshi uliosakinishwa kwenye injini hii.
Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye mafla na eneo la silinda. Kagua mafla kwa
nyufa, kutia kutu, au uharibifu mwingine. Ondoa kifaa cha kusonga au kishika cheche,
iwapo kipo, na ukague kwa uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Iwapo uaribifu utapatikana,
sakinisha sehemu za ubadilishaji kabla ya kuendesha.
Onyo
Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa katika eneo sawa kama
sehemu asili. Sehemu zingine huenda zisitekeleze vilevile, zinaweza kuharibu kitengo,
na inaweza kusababisha majeraha.
Badilisha Mafuta ya Injini
Tazama Kelelezo: 8, 9, 10, 11
Mafuta yaliyotumiwa ni bidhaa taka yenye madhara na lazima itupwe vizuri. Usitupe pamoja
na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha usaidizi au mtoa
huduma kwa utupaji/kutumia upya salama kwa bidhaa.
Ondoa Mafuta
1.
Injini ikiwa imezimwa lakini ina joto, tenganisha waya wa kiziba cheche (D, Kielelezo
8) na uhifadhi mbali na kiziba cheche (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta (A, Kielelezo 9).
Kiziba cha Kutoka Mafuta, iwapo kipo
1.
Ondoa kiziba cha kutoa mafuta (F, Kielelezo 9). Weka mafuta kwenye kontena
iliyoidhinishwa.
Kumbuka: Kuziba cheche yoyote ya kutoa mafuta inaweza kusakinishwa kwenye injini (G,
Kielelezo 9).
2.
Baada ya mafuta kutolewa, sakinisha na ukaze kiziba cha kutoa mafuta (F, Kielelezo
9).
Kitoaji Mafuta cha Haraka, iwapo kipo
1.
Ondoa bomba la kutoa mafuta haraka (H, Kielelezo 10) kutoka upande wa injini.
2.
Geuza na uondoe kifuniko cha kutoa mafuta (I, Kielelezo 10). Teremsha kitoa mafuta
haraka kwa utaratibu (H) katika kontena iliyoidhinishwa (J).
3.
Baada ya mafuta kutolewa, sakinisha kifuniko cha kutoa mafuta haraka (I, Kielelezo
10). Ambatisha bomba la kutoa mafuta haraka (H) kwenye upande wa injini.
Badilisha Kichujio cha Mafuta, iwapo kipo
Baadhi ya modeli zina kichujio cha mafuta. Kwa vipindi vya ubadilishaji, tazama Ratiba
ya Udumishaji.
1.
Toa mafuta kutoka kwenye injini. Tazama eneo la Kuondoa Mafuta .
2.
Ondoa kichujio cha mafuta (K, Kielelezo 11) na ukitupe vizuri.
48
3.
Kabla usakinishe kichujio kipya cha mafuta, lainisha kiasi kwa kifaa cha kichujio cha
mafuta kwa mafuta freshi na safi.
4.
Sakinisha kichujio cha mafuta kwa mkono hadi kifaa kisgusane na adapta ya kichujio
cha mafuta, kisha kaza kichujuio cha mafuta kwa mizunguko 1/2 hadi 3/4.
5.
Ongeza mafuta. Tazama sehemu Ongeza Mafuta .
6.
Washa na uendeshe injini. Wakati injini inachemka, angali uvujaji wa mafuta.
7.
Zima injini na uangalie kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha mafuta kiko juu ya
kiashiria kilichojaa (B, Kielelezo 8) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta.
Ongeza Mafuta
•
Hakikisha kuwa mtambo uko katika kiwango.
•
Safisha eneo la kujaza mafuta kutokana na uchafu wowote.
•
Tazama Vipimo katika eneo la kiwango cha mafuta.
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 8) na upanguse kwa
kitambaa safi.
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la injini (C, Kielelezo 8).
Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza mafuta, subiri dakika moja na kisha angalia
kiwango cha mafuta.
Kumbuka: Usiongeze mafuta kwenye kitoa mafuta haraka (H, Kielelezo 10), iwapo kipo.
3.
Sakinisha na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 8).
4.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta na ukague kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha
mafuta kiko juu ya kiashiria kilichojaa (B, Kielelezo 8) kwenye kifaa cha kuangalia
kiwango cha mafuta.
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 8).
6.
Unganisha waya wa kuziba cheche (D, Kielezo 8) kwenye kuziba cheche (E).
Shughulikia Kichuja Hewa
Tazama Kelelezo: 12
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
•
Kamwe usiwashe na kuendesha wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo kipo)
au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Modeli mbalimbali aidha zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia
zinaweza kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na
kutumiwa tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye
injini yako na ushughulikie kama ifuatavyo.
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 12).
2.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 12).
3.
Ili kuondoa kichujio (C, Kielelezo 12), nyanyua mwisho wa kichujio kisha uvute kichujio
kutoka kwenye eneo la kutia mafuta (E).
4.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio (C, Kielelezo 12) kwenye eneo
gumu. Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
5.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 12), ikiwa kipo, kwenye kichujio (C).
6.
Osha kisafishaji cha mwazo kwenye sabuni oevu na maji, (D, Kielelezo 12). Ruhusu
kisafishaji cha mwanzo kukauka. Usiweke mafuta kwenye kisafishaji cha mwanzo.
7.
Kusanya kisafishaji cha mwanzo kilichokauka (D, Kielelezo 12), ikiwa kipo, kwenye
kichujio (C).
8.
Sakinisha kichujio (C, Kielelezo 12) kwenye eneo la kutiwa mafuta (E). Sukuma
mwisho wa kichujio katika sehemu ya chini. Hakikisha kichujio kinatoshea kwa
usalama katika sehemu ya chini.
9.
Sakinisha jalada (B, Kielelezo 12) na ulinde kwa bizimu(s) (A). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Fanyia huduma Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 13
BRIGGSandSTRATTON.com