KUMBUKA: Ukibonyeza kitufe cha prima sana, injini itafurika na itakuwa gumu
kuiwasha.
6.
Shikilia wenzo wa kuzima injini (C, Kielelezo 9), iwapo upo, dhidi ya kishikio.
7.
Kwa uthabiti shikilia kishikio cha kamba ya kianzishaji (D, Kielelezo 11). Vuta
kamba ya kianzishi polepole hadi uhisi upinzani, kisha vuta haraka.
ONYO
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka) kutavuta
mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia. Inaweza kupelekea
mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo. Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka
wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na
kisha uvute haraka.
Zima Injini
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
•
Usikabe kabureta (iwapo ipo) ili kusimamisha injini.
1.
Achilia wenzo wa kuzima injini (E, Kielelezo 9), iwapo upo.
2.
Sukuma swichi ya kuzima (D, Kielelezo 10), iwapo ipo, hadi kwenye eneo
linaloonyesha ZIMA.
3.
Sogeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 7), iwapo kipo, hadi eneo linaloonyesha
SIMAMA.
4.
Geuza ufunguo wa kianzishaji kwa umeme hadi eneo linaloonyesha ZIMA/
SIMAMA.
5.
Ondoa ufunguo, na uuweke katika mahali salama mbali na watoto.
6.
Baada ya injini kuzima, sogeza vali ya kufunga mafuta (A, Kielelezo 7), iwapo ipo,
hadi eneo linaloonyesha IMEFUNGWA.
Udumishaji
Maelezo ya Udumishaji
ONYO
Wakati wa huduma ya udumisha ikiwa ni muhimu kuinamisha kifaa, ikiwa tangi la
mafuta limeshikana na injini, hakikikisha kwamba ni tupu na upande wa plagi ya spaki
uko juu. Ikiwa tangi la mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au
mlipuko. Ikiwa injini imeinama katika mkao tofauti, haitaguruma kwa urahisi kwa sababu
ya kuchafuka kwa chujio la hewa au plagi ya spaki kwa oili au mafuta.
Tunapendekeza kwamba umwone Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa yeyote wa Briggs &
Stratton ili kupata huduma zote ya udumishaji na kufanyia huduma injini na sehemu za
injini.
NOTISI
Vijenzi vyote vilivyotumiwa kutengeneza injini hii ni lazima visalie kwenye maeneo yake
ili kupata uendeshaji bora.
ONYO
Mwako wa injini usiokusudiwa unaweza kusababisha mshutuko wa umeme au
moto na kupelekea kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha
mabaya ya ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
•
Tenganisha waya wa plagi ya spaki na uuweke mbali na plagi ya spaki.
•
Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishaji cha umeme.)
•
Tumia zana sahihi pekee.
Unapokagua uwepo wa cheche:
•
Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
•
Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Ili kupata huduma ya udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo
ya kudhibiti mafukizo, wasiliana na kituo chochote kinachohitimu cha kukarabati
injini au mtoa huduma aliyehitimu wa kukarabati injini. Hata hivyo, ili kupata
huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na muuzaji
aliyeidhinishwa na kiwanda. Rejelea Kauli za Udhibiti Mafukizo.
Ratiba ya Udumishaji
Saa 5 za Kwanza
Badilisha oili ya injini (haihitajiki kwenye miundo iliyo na lebo ya Just Check &
•
™
Add
na Hakuna Kubadilisha Oili).
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
•
Kagua kiwango cha oili ya injini.
•
Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla na vidhibiti.
•
Safisha grili ya kuingiza hewa.
Kila Baada ya Saa 25 au Kila mwaka
•
1
Safisha chujio la hewa
.
•
Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo)
Kila Baada ya Saa 50 au Kila mwaka
•
Badilisha oili ya injini (haihitajiki kwenye miundo iliyo na lebo ya Just Check &
™
Add
na Hakuna Kubadilisha Oili).
Kila Mwaka
•
Badilisha plagi ya/za spaki.
•
Badilisha chujio la hewa.
•
Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo).
•
Fanyia huduma mfumo wa kupoesha
•
2
Kagua uwazi wa vali
.
1
Safisha mara nyingi zaidi katika mazingira ya vumbi au wakati kuna vipengee vingi
hewani.
2
Haihitajiki isipokuwa kutokee matatizo ya utendakazi wa injini.
Kabureta na Kasi ya Injini
Usifanye marekebisho kwenye kabureta au kasi ya injini. Kabureta ilifungwa kiwandani
ili kufanya kazi kwa ufanisi katika mazingira mengi. Usihitilafiane na springi ya kidhibiti,
viunganishaji, au sehemu nyingine ili kubadilisha kasi ya injini. Iwapo marekebisho
yoyote yanahitajika, wasiliana na Mtoa Huduma Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili
kufanyiwa huduma.
NOTISI
Mtengenezaji wa kifaa hubainisha kasi ya juu zaidi ya injini kama ilivyosakinishwa
kwenye kifaa. Usizidishe kasi hii. Iwapo huna uhakika kasi ya juu zaidi ya kifaa hiki
ni ipi, au kasi ya injini iilivyopangwa tangu kiwandani, wasiliana na Muuzaji Huduma
Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata usaidizi. Kwa oparesheni salama na
sahihi ya kifaa hiki, kasi ya injini inapaswa tu kurekebishwa na mtaalamu wa huduma
aliyehitimu.
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafukizo
ONYO
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Vitu vinavyoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi, vinaweza kushika
moto.
•
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
•
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442, kutumia
au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi, au
lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama ilivyobainishwa katika
sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka nyingine
za majimbo au serikali ya kitaifa huenda zikawa na sheria sawia; Rejelea Kanuni za
Serikali ya KItaifa ya 36 CFR Sehemu ya 261.52. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa
kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya
mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
Ondoa vifuzi vilivyokusanyika kutoka kwenye mafla na eneo la silinda. Kagua mafla
kama ina nyufa, ubabuzi, au uharibifu mwingine. Ondoa kifaa cha kusonga au kishika
cheche, iwapo kipo, na ukague kama kuna uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Iwapo
uharibifu utapatikana, sakinisha sehemu za ubadilishaji kabla ya kuendesha kifaa.
ONYO
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo sawa
kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au kusababisha
majeraha.
1
.
1
.
55