iwapo kipo, na ukague kwa uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Iwapo uaribifu utapatikana,
sakinisha sehemu za ubadilishaji kabla ya kuendesha.
Onyo
Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa katika eneo sawa
kama sehemu asili. Sehemu zingine huenda zisitekeleze vilevile, zinaweza kuharibu
kitengo, na inaweza kusababisha majeraha.
Badilisha Mafuta ya Injini
Tazama Kelelezo: 9, 10, 11
Mafuta yaliyotumiwa ni bidhaa taka yenye madhara na lazima itupwe vizuri. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha usaidizi
au mtoa huduma kwa utupaji/kutumia upya salama kwa bidhaa.
Ondoa Mafuta
1.
Injini ikiwa bado ina joto, tenganisha waya ya kuziba cheche na uihifadhi mbali na
kuziba cheche (E) (D, Kielelezo 9).
2.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta (A, Kielelezo 10).
3.
Ondoa kiziba cha kutoa mafuta (F, Kielelezo 11). Weka mafuta kwenye kontena
iliyoidhinishwa.
4.
Baada ya mafuta kutolewa, sakinisha na ukaze kiziba cha kutoa mafuta (F,
Kielelezo 11).
Badilisha Kichujio cha Mafuta, iwapo kipo
Baadhi ya modeli zina kichujio cha mafuta. Kwa vipindi vya ubadilishaji, tazama Ratiba
ya Udumishaji.
1.
Toa mafuta kutoka kwenye injini. Tazama eneo la Kuondoa Mafuta .
2.
Ondoa kichujio cha mafuta (G, Kielelezo 11) na ukitupe vizuri.
3.
Kabla usakinishe kichujio kipya cha mafuta, lainisha kiasi kwa kifaa cha kichujio
cha mafuta kwa mafuta freshi na safi.
4.
Sakinisha kichujio cha mafuta kwa mkono hadi kifaa kisgusane na adapta ya
kichujio cha mafuta, kisha kaza kichujuio cha mafuta kwa mizunguko 1/2 hadi 3/4.
5.
Ongeza mafuta. Tazama sehemu Ongeza Mafuta .
6.
Washa na uendeshe injini. Wakati injini inachemka, angali uvujaji wa mafuta.
7.
Zima injini na uangalie kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha mafuta kiko
juu ya kiashiria kilichojaa kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (B,
Kielelezo 10) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta.
Ongeza Mafuta
• Hakikisha kuwa mtambo uko katika kiwango.
• Safisha eneo la kujaza mafuta kutokana na uchafu wowote.
• Tazama Vipimo katika eneo la kiwango cha mafuta.
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 10) na upanguse
kwa kitambaa safi.
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la injini (C, Kielelezo 10).
Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza mafuta, subiri dakika moja na kisha
angalia kiwango cha mafuta.
3.
Sakinisha na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 10).
4.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta na ukague kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi
cha mafuta kiko juu ya kiashiria kilichojaa kwenye kifaa cha kuangalia kiwango
cha mafuta (B, Kielelezo 10) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta.
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo
10).
6.
Unganisha waya ya kuziba cheche kwenye kuziba cheche (E), (D, Kielelezo 9).
Shughulikia Kichuja Hewa
Tazama Kelelezo: 12, 13
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
• Kamwe usiwashe na kuendesha wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo
kipo) au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Modeli mbalimbali aidha zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia
zinaweza kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na
kutumiwa tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye
injini yako na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Fungua bizimu (A, Kielelezo 12) na uondoe kifuniko (B).
2.
Ondoa kichujio cha hewa (C, Kielelezo 12).
3.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio cha hewa katika eneo gumu.
Iwapo kichujio cha hewa ni kichafu kupita kiasi, badilisha kwa kichujio kipya cha
hewa
4.
Ondoa kichujio cha usalama (D, Kielelezo 12), iwapo kipo, kivute kwa utaratibu
kutoka kwenye mwili wa kisafishaji cha hewa (E). Hakikisha kuwa uchafu au
mabaki hayaingii kwenye mtambo.
5.
Sakinisha kichujio cha usalama (D, Kielelezo 12) katika mwili wa kisafishaji cha
hewa (E).
6.
Sakinisha kichujio cha hewa (C, Kielelezo 12) kwenye kichujio cha usalama (D).
7.
Sakinisha jalada (B, Kielelezo 12) na ufunge bizimu (A).
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Ondoa bizimu (A, Kielelezo 13).
2.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 13).
3.
Ondoa bizimu (C, Kielelezo 13) na kishikiliaji (D).
4.
Ondoa kichujio cha hewa (E, Kielelezo 13).
5.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (F, Kielelezo 13), iwapo kipo, kutoka kwenye
kichujio cha hewa (E).
6.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio cha hewa (E, Kielelezo, 13)
kwenye eneo gumu. Iwapo kichujio cha hewa ni kichafu kupita kiasi, badilisha kwa
kichujio kipya cha hewa
7.
Osha kisafishaji cha mwanzo (F, Kielelezo 13), iwapo kipo, kwenye sabuni oevu
na maji. Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta
kwenye kisafishaji cha mwanzo.
8.
Sakinisha kisafishaji cha mwanzo kilichokauka (F, Kielelezo 13), ikiwa kipo,
kwenye kichujio cha hewa (E).
9.
Sakinisha kichujio cha hewa (E, Kielelezo 13) na kuweka salama kwa kishikiliaji
(D) na bizimu (C).
10.
Sakinisha jalada (B, Kielelezo 13) na ulinde kwa bizimu(s) (A). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Fanyia huduma Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 14
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
• Kagua njia za mafuta, tangi, kifuniko na sehemu nyingine mara kwa mara ili uone
kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha kama itahitajika.
• Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta, mimina mafuta kutoka kwa
tangi ya mafuta au ufunge vali ya kuzuia mafuta.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatavukiza kabla ya kuwasha
injini.
• Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa kwa namna sawa na
sehemu asili.
Kichujio cha Mafuta, iwapo kipo
1.
Kabla ya kubadilisha kichujio cha mafuta (A, Kielelezo 14), iwapo kipo, mimina
mafuta kutoka kwa tangi la mafutai au funga vali ya kuzuia mafuta . La sivyo,
mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
2.
Tumia koleo kubana vichupo (B, Kielelezo 14) kwenye vibanio (C), ) kisha
telezesha vibanio kutoka kwenye kichujio cha fueli (A). Zungusha na uvute njia za
mfuta (D) kutoka kwenye kichujio cha mafuta.
3.
Kagua njia za mfuta (D, Kielelezo 14)ili uone kamakuna nyufa au uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
4.
Badilisha kichujio cha mafuta (A, Kielelezo 14) kwa kichujio halisi cha kubadilisha
sehemu.
45